WANAFUNZI ELFU 4 NI WAJAWAZITO PWANI


Zaidi ya wanafunzi elfu 4 wa kike hapa Pwani ni wajawazito  tangu kufungwa kwa shule kwa sababu ya ugonjwa wa COVID 19.
Haya ni kulingana na mshirikishi wa Kanda ya  Pwani John Elungata ambaye amesema kuwa visa hivyo vimeripotiwa kati ya mwezi Machi na Juni mwaka huu.
Kwenye takwimu hizo, kaunti ya Kilifi inaongoza kwa visa 3,376 huku kaunti ya Mombasa ikinakili visa  941 na kaunti nyengine zikifuata.
Wakati huo huo amedokeza kuwa waathiriwa ni Wanafunzi wa kati ya umri wa miaka 10 hadi 19 ambao hudanganywa na watu wanaowapachika mimba hali aliyoitaja kuwa ya kusikitisha akiwataka wazazi kuchukua majukumu ya kuona kuwa watoto wao wanapata mahitaji yao.
Aidha amewataka viongozi wa kidini kuhamasisha jamii kuwalinda mabinti wao haswa wakati huu ambapo shule zimefungwa hadi mwaka ujao ili kuwaepusha na mimba za mapema.