WANABODABODA WATAKIWA KUWA MAKINI-CORONA


Wito umetolewa kwa wanabodaboda kaunti ya Taita Taveta kuwa makini wanapobeba abiria na kutakiwa kuzingatia usafi wakati taifa hili linashuhudia visa vya virusi vya Corona.

Kulingana na mwenyekiti wa wanabdaboda nchini Kelvin Mbadi anasema ni sharti wanabodaboda kutotumiwa kupitisha watu katika vichochoro vya mpakani na badala yake kuhakikisha abiria wanaowabeba wamekaguliwa.
Mbandi anasema sekta hiyo ni muhimu kwa usafiri hapa nchini na sharti mikakati iwekwe kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona