WAMILIKI WA MASHAMBA KUHUSU UWINDAJI HARAMU,TAITA TAVETA.


Huku Serikali ya kaunti ya kaunti ya Taita Taveta ikiendela kusutwa kwa kushindwa kuwakabili walishaji haramu na mifugo yao, sasa imebainika kuwa walishaji hao wamekuwa wakijihusisha na uwindaji haramu japo kisiri.

Mwenyekiti wa shamba kubwa la kukodi kaunti hiyo John Msabaa anasema kuwa ,walishaji hao wanafaa kufurushwa ikizingatiwa kuwa ni tishio kwa usalama.

Aidha anatoa wito kwa serikali hiyo kukumbatia ushauri wa mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime ,wa kuwaajiri vijana kama askari jamii ambao watakuwa wakipiga doria sehemu mbali mbali za kaunti hiyo.