WALIMU WA SHULE ZA KIBINAFSI MTOPANGA MOMBASA WAPEWA CHAKULA CHA MSAADA


Serikali ya kaunti ya Mombasa imeanzisha zoezi la kuwapa chakula cha msaada walimu kutoka shule za kibinafsi mjini Mombasa baada ya kubaini kwamba baadhi yao wamekuwa wakipitia changamoto chungu nzima baada ya kufungwa kwa shule.

Akizungumza kwenye zoezi hilo katika eneo la Mtopanga kwenye eneo bunge la Kisauni Mombasa, Naibu gavana wa kaunti ya Mombasa William Kingi amesema kwamba kamati iliyotwikwa jukumu la ugavi wa chakula Mombasa imebaini kuwa miongoni mwa waliothirika pakubwa ni walimu wa shule za kibinafsi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa walimu katika shule za kibinafsi Mombasa Omari Mbudi amesema kwamba zaidi ya shule mia moja za kibinafsi Mombasa zimefungwa na wamiliki wa majengo hayo baada ya wasimamizi kushindwa kulipa tangu kuibuka kwa janga la Corona.