Walimu Baringo waelezea wasiwasi kuhusu Covid-19 shuleni


Baadhi ya walimu katika kaunti ya Baringo wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na ongezeko la visa vya corona shuleni.

Kupitia kwa Naibu katibu wa muungano wa walimu wanawake nchini KEWOTA,Charity Ng’eno, walimu hao wameitaka wizara ya eliku kusaidia shule zilizoathirika ili kuzuia kuenea kwa maamukizi zaidi.

Ngeno ameelezea haja ya serikali kuwasaidia walimu na wanafunzi walioathiriwa na virusi vya corona hasa kugharamia maeneo ya karantini.

Walimu hao aidha wameeelzea wasiwasi kutokana na ongezeko la visa vya mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi hasa wakati huu wako nyumbani kwa likizo ndefu.