WALEMAVU HADI SASA HAWAJAHUSISHWA.

Walemavu katika kaunti ya Lamu wamehuzunishwa kuona hadi sasa jamii ya walemavu Lamu hawajapewa miradi ya kujihusisha na kazi mtaaani ili wapate kujimudu kimaisha.
Mwakilishi wa walemavu Ikhwan Omar ametaka serikali kuu kuweka wazi mipangilio waliyopangia jamii inayoishi na ulemavu ili na wao wapate ajira sawa na wasokuwa walemavu.
Kazi mtaani inayoendelea kaunti ya Lamu vijana walemavu hawajahusishwa kwenye mpango huo kwa kile kilichotajwa kwamba ni kazi ngumu ambazo hawawezi kuzifanya.
Kulingana na Omar walemavu wengi wamesalia majumbani wakiendelea kukabiliwa na hali ngumu za kimaisha kutokana na serikali kuu sawa na serikali ya kaunti kuwasahau katika mipangilio ya nafasi za kazi.