WAKULIMA WASAIDIWE NA SERIKALI


Idara za serikali kaunti ya Taita Taveta zimetakiwa kuhakikisha zinatumia fedha za bajeti yake katika kufundisha wakulima kilimo cha kisasa.

Wakulima wanasema mara kwa mara fedha zinazotengwa zimekuwa haziwafaidi licha ya maafisa wa serikali kupewa jukumu la kuhudumia wananchi.
Wito wao unajiri wakati huu ambapo bajeti ya mwaka 2020/2021 ilipitishwa juma lililopita huku kukiwa na miradi katika sekta ya kilimo ambayo haijakamilika.