Wakulima wa ngombe wa maziwa watabasamu Kilifi.


Wakaazi wa wadi ya ganda sasa wanayo sababu ya kutabasamu baada ya serikali ya kaunti ya Kilifi kununua jumla ya ng’ombe 58 kwa wakulima wafugaji eneo hilo.

Taarifa zimefichua kuwa Serikali ya kaunti ya Kilifi imetumia jumla ya shilingi milioni 10 kwa ununuzi wa ng’ombe hao wa maziwa.

Kulingana na mwakilishi wadi ya Ganda Reuben Katana mradi huo unanuiya kuimarisha kilimo cha ufugaji na uchumi miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo.

Fauka ya hayo Katana amedokeza kuwa hatua hiyo pia itaboresha hata Zaidi afya ya wakaazi kwa kupata maziwa pomoni.

Amewahauri wakaazi walionufaika na mradi huo kuhakikisha wanazingatia mafundisho walipewa kuhusu mbinu za kuwafuga ng’ombe hao ikiwemo kuwadunga sindano na pia kuwaosha mara kwa mara.

Katana amewakumbusha wakaazi wa eneo hilo kuzingatia maagizo yote ya wizara ya afya yanayolenga kupunguza kusambaa kwa virusi vya Corona.

Hata hivyo baadhi ya wakaazi walionufaika na mradi huo wakiongozwa na Christine Mlewa, wameupongeza mradi huo wakiahidi kuzingatia maagizo ya wizara ya kilimo kuhusu ufugaji wan ng’ombe hao wa kisasa.