Wakongwe kuanza kulipwa Jumatatu


Serikali imewasilisha shilingi bilioni 4.3 zitakazotumika kuwalipa wakongwe na mahitaji ya kimsingi katika jamii kuanzia kesho.

Katibu anayesimamia idara hiyo Nelson Marwa anasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wanatarajiwa kunufaika na pesa hizo, wakijumuisha mayatima zaidi ya 295,000 wanaotarajiwa kupokea shilingi bilioni 1.1 huku wakongwe wazaidi ya 700,000 wakipokea shilingi bilioni 3.

Marwa anasema kuwa kila mmoja atapokea shilingi 4,000 za mwezi Novemba na Desemba mwaka jana.