WAKAIDI MAAGIZO YA KORONA, KWALE.


Watu wanane kati ya kumi na wawili waliokamatwa na polisi ,wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha kinango kaunti ya kwale ,kwa kukaidi agizo la wizara ya afya la kuvaa barakoa ,ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa Ocpd eneo la kinango Fredrick Ombaka ,12 hao waliokamatwa mjini kinango, ni wa kati ya umri wa miaka 21 hadi 59 .

Vile vile ameeleza kwamba wanne kati yao ,walio zaidi ya umuri wa miaka 50 wameachiliwa ,huku wakionywa vikali dhidi ya ukiukaji wa agizo hilo, kuwa wakipatikana kwa mara nyingine watakabiliwa kisheria.

Hata hivyo 8 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya jumatatu ,huku msako wa kuvaa barakoa ukiendelea.