Wakaazi watoa maoni kuhusu mswada wa BBI Mombasa.


Wakaazi katika kaunti ya Mombasa hii leo wameanza zoezi la kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu mwada wa BBI baada ya mswada huo kuwasilishwa katika bunge la kaunti ya Mombasa majuma mawili yaliyopita.

Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea kwa siku mbili ambapo hii leo wakaazi katika maeneo bunge ya Mvita, Nyali na Kisauni wanaendelea kutoa maoni yao, huku maeneo ya Likoni Changamwe na Jomvu yakitarajiwa kuliziungumzia hapo kesho Ijumaa.

Maoni hayo ya wananchi hatimaye yatakusanywa na kisha kuwasilishwa katika bunge la kaunti ya Mombasa inayotarajiwa kujadili mswada huo juma lijalo na kisha kuuangusha au kuupitisha.

Hadi kufikia sasa tayari kaunti nane zimejadili mswada huo bungeni ambapo kaunti saba ikiwemo Homabay, Kisumu, Busia, Pokot Magharibi, Trans Nzoia na Kajiado wamepitisha mswada huo huku kaunti ya Baringo ikiuangusha.