WAKAAZI WATAKIWA KUTOEKEANA CHUKI LAMU.


Naibu gavana wa kaunti ya Lamu Abdul Hakim Aboud ametoa wito kwa wakaazi kutokosa matumaini iwapo wamefeli katika maisha yao na badala yake kujizatiti na  kujituma ili wafanikiwe .

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Hakim ametoa nasaha kwa wakaazi iwapo wamekosana na watu wengine kusameheana na kuangalia maisha ya mbeleni badala ya kuekeana chuki moyoni.

Haya yanajiri huku kukishuhudiwa chuki na uhasama baina ya viongozi katika kaunti ya Lamu kutokana na mirengo  ya kisiasa kuhusu uchaguzi wa mwaka 2022.