WAKAAZI WAONYWA DHIDI YA UVAMIZI WA MASHAMBA,TAITA TAVETA.


Serikali imeonya vikali wananchi dhidi ya kuvamia mashamba ya watu binafsi na kuanza kugawanya vipande kwa ajili ya ukulima.

 
Kulingana na kaunti kamishna wa Taita Taveta Rhoda Onyancha anasema kama serikali hawatakubali wachochezi wa ardhi na kwamba watakaovamia mashamba ya wenyewe hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
Onyancha anasema kuna baadhi ya watu kaunti hiyo ambao wanajifanya kuwa maskwota ili wapate ardhi za bure.