Wakaazi walalamikia uwepo wa pikipiki Lamu.


Wakaazi wa Kisiwa cha Lamu wanaendelea kulalamika kwamba ujio wa pikipiki Kisiwani Amu umechangia pakubwa watalii wengi ikiwemo watalii ambao ni wakaazi wa Lamu kuhama maeneo hayo.

Kulingana na Wakaazi wamesema Kisiwa cha Amu ni mji mdogo na barabara za mji huo ni nyembamba zilizojengwa karne kwa minajili ya matumizi ya punda,mikokoteni sawa na watu kutembea pekee.

Mwaka 2017 Kisiwa cha Amu kilikuwa na pikipiki 20 pekee ila kufika sasa Kisiwa hicho kina pikipiki Zaidi ya 300 ambazo zimekuwa kero kubwa kwa wageni na ata wakaazi.

Aidha wakaazi wameishtumu vikali serikali ya kaunti ya Lamu sawa na serikali kuu kwa kukosa kudhibiti pikipiki hizo.