Wakaazi walalamikia Umeme Lamu.


Wakaazi katika eneo la Ndeu _Hindi kaunti ya lamu wamehuzunishwa kuona kwamba licha ya kuwa wao wanaoshi karibu na kituo cha kusambaza umeme lakini wamesalia kwenye giza.

 

Kulingana na wakaazi hao miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakitumia taa za chemni na vikoroboi licha ya kuwa na kituo cha umeme eneo lao,umeme ambao umesambazwa maeneo mengi ya Hindi.

Aidha wametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuwasaidia na kuwavutia moto w umeme ili wapate huduma za kimsingi kama sehemu zengine.

Wamebaini kuwa eneo hilo mara kwa mara kumeshuhudiwa changamoto za usalama, wizi wa mara kwa mara kutokana na ukosefu wa mwangaza.