WAKAAZI WALALAMA KUHUSU UKOSEFU WA MAJI


Serikali ikisistiza Wakenya kunawa mikono kila wakati mojawapo ya njia za kukabili kusambaa kwa virusi vya korona , sasa wakazi wa vijiji vya Peleleza  na Kariobangi mjini Mwatate kwenye kaunti ya Taita Taveta wamelalamikia ukosefu wa bidhaa hiyo .

Wanasema huenda agizo la serikali lililotolewa na waziri wa afya Mutahi Kagwe likakosa kuafikiwa kwani licha ya kupiga ripoti kwa wizara husika uhaba wa bidhaa hiyo ungalipo.

Kuafuatia hali hiyo sasa wamewasuta viongozi wa eneo hio kwa kukosa kuwajibika na kumshinikiza waziri husika kusambaza maji katika vijiji hivyo.

Ni hali aidha imeshuhudiwa sehemu mbali mbali za mashinani za kaunti hiyo hasa maeneo ya Mwakitau, Chungaunga, Mbololo, Mgeno miongoni mwa maeneo mengine.