WAKAAZI WAKOSA HUDUMA ZA MAJI-TAITA TAVETA


Kwa siku ya tatu mfululizo wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta na hasa mjini Voi na viunga vyake wamekosa huduma za maji kutoka kwa shirika la usambazaji maji la Tavevo.
 
Hii inafuatia kupasuka kwa bomba kuu la maji la mzima huku tayari athari za kukosekana kwa maji zikionekana mjini Voi huku vyoo ya umma zikisalia kufungwa.
 
Aidha maeneo mengine kama vile Maungum,Msharinyi,Miasenyi sawa na Macknon Road wakaazi sasa wanalazimika kutafuta maji katika mabwawa huku wakihofia mkurupuko wa magonjwa.
 
Haya yanajiri huku serikali ya kaunti hiyo ikisisitiza kwamba watafanya mipango maalum ili wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi iweze kupata maji kwa kutumia malori maalum ya kubebea maji.