Wakaazi wa Watamu walilia ardhi yao inayodaiwa kunyakuliwa.


Hali ya taharuki imetanda katika eneo la Watamu kufuatia madai ya kuvamiwa kwa ardhi katika kijiji hicho na bwenyenye mmoja.

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo jumla ya watu 3,000 wameathirika na uvamizi huo wa ardhi ambao huenda ukasambaratisha amani eneo hilo.