Wakaazi wa Uasin gishu waonywa kuhusu Corona


Gavana wa Uasin Gishu ameendelea kuwahimiza wenyeji wa kaunti hiyo kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona baada ya idadi ya wanaougua ugonjwa wa Covid-19 kuongezeka kwa kiwango kubwa katika kaunti hiyo ya Uasin Gishu.

Anasema kwamba ni jambo la kusikitisha kuona kwamba idadi kubwa ya watu hawavalii barakoa wakiwa katika maeneo ya umma huku wengine wakokosa kunawa mikono hali anayosema imechangia pakubwa ongezeko la visa vya corona eneo hilo.

Akizungumza kule Eldoret Mandago amesema vita dhidi ya corona vitafaulu humu nchini iwapo wakenya wote watawajibika kwa kufuata masharti yote yaliyowekwa na wizara ya afya.