WAKAAZI WA MWATATE NA WITO KWA MWEKEZAJI KUHESHIMU MAAGIZO YA MAHAKAMA


Wakaazi wa Mwatate wamelalamikia hatua ya mwekezaji wa kibinafsi eneo hilo ,kuanza kupima ardhi ya shamba licha ya shamba kuwa na kesi mahakamani.

Wakaazi hao wakiongozwa na mwanaharakati Mnjala Mwaluma anasema ,masorovea wa kibinafsi wamekuwa wakipima ardhi ,licha ya kwamba kesi inayokabili shamba hilo, itasikilizwa mwezi wa tano mwaka huu.

Kwa sasa wanatoa wito kwa viongozi wa serikali ya kaunti ya Taita Taveta, kuingilia kati mzozo huo ambao umesababisha wakaazi zaidi ya elfu moja kuwa maskwota.