WAKAAZI WA MTAA WA STADIUM NA LALAMA ZA MIRUNDIKO YA TAKA,KWA KUHOFIA MKURUPUKO WA MARADHI.


 

Wakaazi wanaoishi katika mtaa wa Stadium , Tononoka kaunti ya Mombasa wanalalamika kuhusu kujaa kwa taka nje ya uwanja wa michezo wa Mombasa unaoendelea kujengwa.

Taka hizo zimepakana na mabati ambayo yamezingira uwanja huo ,huku
wakisema wamelazimika kuishi na harufu ya uvundo pamoja kusumbuliwa na mamia ya ndege aina ya kunguru na hata tumbili wakiwa wanapiga kambi kwenye eneo hilo.

Wakisema kuwa kuna hofu ya mkurukupo wa maradhi yanayosababishwa na taka hizo na kuitaka serikali ya kaunti kuchukua hatua na kuondoa taka hizo ambazo sasa zimekuwa kero kwao.