Wakaazi wa Msambweni wapinga wito wa Haki afrika kutaka uchaguzi mdogo kuhairishwa.


Baadhi ya wakaazi wa eneo la Msambweni kaunti ya kwale wamepinga hatua ya shirika la kutetea haki za kibinadmu Haki Afrika kutaka uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni uhairishwe kwa madai kuwa kampeni za wagombea hazizingatii masharti ya kukabili msambao wa virusi vya corona.

Wakiongozwa na Mshenga Vuya Ruga wakaazi hao wanaesema kuwa wamesubiri kwa kipindi cha miezi sita kupata uwakilishi bungeni tangu kuaga kwa Suleimani Dori mwezi Machi mwaka huu, na wanataka shirika hilo kusitisha juhudi za kusimamisha uchaguzi huo.