WAKAAZI WA LAMU WATAKIWA KUUNGA MKONO ZOEZI LA KUPEWA HATI MILIKI.


Wakaazi katika kaunti ya Lamu wametakiwa kuunga mkono zoezi linaloendelezwa na serikali ya kaunti hiyo, la kuwapa wakaazi hatimiliki ili kupata kumiliki ardhi zao.

Waziri wa ardhi kaunti ya Lamu Fahima Araphat ,amesema wakaazi wanapokuwa na hatimiliki zao ,wataweza kuuza ardhi hizo kwa bei ya juu kando na inavyoshuduhiwa kwa sasa.

Fahima ametoa mfamo wa wakaazi ambao hawakuwa na hatimiliki ,waliokuwa wanaishi katika ardhi ya bandari ya Lamu eneo la KILI LANA, kwamba walipewa fidia finyu kutokana na wao kukosa kuwa na hatimiliki ,ikizingatiwa ni ardhi iliyo baharini.