WAKAAZI WA LAMU NA SEHEMU YA KUTUPA TAKA.


Wakaazi wa eneo la Kiunga kaunti ya Lamu wameitaka serikali ya kaunti hiyo kuweka mikakati ya kutenga sehemu ya kutupa taka Kiunga ili kuboresha mazingira ya eneo hilo.
Ismail Omar amesema wakaazi wengi wamekuwa wakitupa taka katika ufuo wa bahari kutokana na ukosefu wa sehemu maalum ya kutupa taka jambo ambalo amelitaja kuharibu sehemu za mazalio ya samaki .
Kwa upande wake Shariff Mohammed ambaye ni miongoni mwa vijana wa eneo hilo amemtaka gavana wa kaunti hiyo Fahim Twaha kuwaajiri vijana katika mpango wa kazi mitaani.
 Shariff amesema kaunti ingewatumia vijana wa eneo hilo kusafisha maeneo ya miji  ili waweze kujitoa katika maswala ya uhalifu na utumizi wa dawa za kulevya.