WAKAAZI WA FAZA NA LALAMA YA HUDUMA DUNI ZA AFYA,LAMU.


Wakaazi katika eneo la Faza Kisiwa cha Pate wamehuzunishwa kuona hospitali ya Faza ambayo ni hospitali ya eneo bunge la Lamu Mashariki, haina vifaa vyovyote vile vya matibabu.

Kulingana na wakaazi hao wagonjwa katika eneo hilo hulazimika kusafirishwa hadi hospitali Kisiwa cha Amu ili kupata matibabu , hali ambayo inahatarisha maisha yao haswa wakati huu ambapo bahari inashuhudia upepo na mawimbi makali.

Aidha wito umetolewa kwa serikali ya kaunti ya Lamu, kuekeza vifaa vya matibabu katika hospitali ya Faza ,ili wagonjwa katika eneo hilo wapate matibabu kwa wakati ufaao.