WAKAAZI LAMU WAPUNGUZE SAFARI ZISIZOMSINGI ILI KUZUIYA MAAMBUKIZI YA CORONA.


Wakaazi katika kaunti ya Lamu wametakiwa kupunguza safari za mara kwa mara zisizokuwa na ulazima kutoka nje ya kaunti hiyo ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya korona.

Kadhalka wazazi wametakiwa kuchukua majukumu yao ipasavyo na kuwalinda wanawao ili wasipate msambao wa virusi hivyo.

Kwa upande wazee sawa na watu walio na magonjwa mengine ya kiafya wametakiwa kusalia majumbani mwao kwani wao ni rahisi na haraka kupata virusi hivyo.

Kaunti ya Lamu kufikia sasa kuna watu takriban 30 waliopata virusi vya korona takwimu zilizotokana na sampuli zaidi ya 400 za wakaazi waliofanyiwa vipimo