WAKAAZI LAMU HAWAZINGATII KANUNI ZA COVID.


Wakaazi katika kaunti ya Lamu wanahofia Idadi ya maambukizi ya virusi vya korona ikaongezeka kwa kiwango kikubwa katika kaunti hiyo  kutokana na mienendo ya wengi wanavyoishi ambapo hawazingatia maagizo ya serikali.

Hii ni baada ya kubainika kuwa wakaazi wengi wamekuwa wakisalimiana kwa mikono,wakikusanyika vibarazani huku wakikosa kuvaa barakoa kutokaa na ukosefu wa hamasisho la kutosha kuhusua hatari za virusi hivyo..

Kulingana na wakaazi , idadi ya watu wote wa Lamu ni wachcahe na kwamba kuna hatari kubwa iwapo virusi hivyo vitasambaa kwa watu wengi.