WAKAAZI KUJIFUNIKA MDOMO WANAPOKOHOA


Wakaazi katika kaunti ya Lamu wametakiwa wanapotaka kuchemua au kukohoa kujifinika midomo yao kwa kutumia kitambaa au tissure na kisha kitamba hicho kukitupa.

Afisa wa afya Nderitu Muteru Lamu amesema itakuwa ni jambo la kuchangia kusambaza virusi vya Korona iwapo mmoja atakohoa kwa kujifinika kitambaa na hatimaye kitambaa hicho kukiweka ndani ya mfuko wake .

Kadhalka amewasihi wakaazi kufata maagizo yaliyowekwa na serikali dhidi ya kujikinga na virusi vya korona  ikiwemo kuketi umbali wa mita moja na mwengine ili kuepukana na usambazaji wa gonjwa hilo.

Haya yanajiri huku idadi ya watu waliothibitishwa kuathirika na virusi vya korona humu nchini ikifikia watu 31.