WAKAAZI KILIFI WALALAMIKIA KUHANGAISHWA NA MABWENYENYE WA UNYAKUZI WA ARDHI .


 

Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Kilifi wamelalamikia vikali kile walichokitaja kama kuhangaishwa na mabwenyenye wenye hulka ya kunyakua ardhi na ulanguzi wa mihadarati eneo hilo.

Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Shimo la Tewa Sammy Ndago ,wakaazi hao wamesema mabwenyenye hao wamekuwa wakitumia maafisa wa polisi kutekeleza hayo.

Kulingana na Mahmud Hambali mmoja wa wakazi mjini Kilifi ,uuzaji wa dawa za kulevya sasa unafanyika hadharani, huku maafisa wa usalama wakikosa kushughulikia swala hilo.

Naye Kamishna wa kaunti ya Kilifi Olaka Kutswa ameeleza kughadhabishwa kwake na hatua hiyo ,na kuwataka maafisa tawala katika eneo hilo kukabiliana na swala hilo mara moja.