WAKAAZI BUXTON WAPINGA MRADI WA NYUMBA


Baadhi ya wakaazi katika mtaa wa Buxton Mombasa sasa wanatishia kwenda mahakamani kupinga mpango wa kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba katika mtaa huo.

Wakaazi hao kupitia katibu mkuu Baya Mwanyule wanasema kwamba nyumba hizo zitakuwa ghali mno na kamwe hawataweza kuzinunua baada ya kukamilika.

Wakaazi hao kwa upande mwingine wanadai kwamba zoezi za kuchukua maoni ya wananchi halifanyiki kwa njia ya uwazi kwa madai kwamba ni wafanyikazi wa kaunti wanaoishi kwenye nyumba hizo wanaohusishwa kwa mazungumzo.

Haya yanajiri huko mkaazi Robert Abwoge akidai kwamba hawataweza kutimiza masharti ya kununua nyumba hizo ikiwemo kutenga takriban shilingi laki sita kama malipo ya mwanzo kabla ya kutengewa nyumba.