Waititu kubaini hatma yake Jumanne ijayo


Hatma ya gavana wa Kiambu Ferdinand waititu Babayao inatarajiwa kujadiliwa jumanne na Jumatano juma lijalo.

Hii ni baada ya spika wa senate Ken Lusaka kuchapisha rasmi siku hizo mbili kutumika kwa mjadala huo unaohusiana na hoja ya kumtimua mamlakani.

Bunge hilo la senate lilifutilia mbali mpango wa hoja hiyo kuangaziwa na kamati maalum na badala yake ishughulikiwe na bunge zima.

Hii ni baada ya mgawanyiko mkubwa kuibuka kuhusu orodha ya maseneta waliofaa kupewa jukumu hilo siku ya jumanne juma hili.