Waiguru ajitetea shahidi wake akitolewa kijasho


Shahidi wa kwanza wa gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amekanusha madai kuwa Gavana aliunda kamati ya kuangazia zabuni kwa njia isiyo halali.

Joseph Otieno anayehudumu kama mkurugenzi wa usimamizi wa uagizaji katika kaunti hiyo anasema kuwa gavana hana usemi katika shughuli ya kuangazia zabuni,afisa wa uhasibu akitwikwa jukumu hilo.

Hata hivyo, Otieno ametolewa kijasho na wakili wa bunge la kaunti Ndegwa Njiru anayetilia shaka baadhi ya ushahidi aliowasilisha kuhusiana na zabuni iliyolewa na serikali ya kaunti hiyo.

Baadaye kamati hiyo ya maseneta 11 itafunga vikao kuandaa ripoti ya mwisho hapo kesho kabla ya kuwasilisha mapendekezo siku ya ijumaa.