WAHUDUMU WA WAFYA LAMU WASEMA FEDHA ZA BBI ,ZINGETUMIKA KUTATUA MATAKWA YAO.


Wahudumu wa afya kaunti ya Lamu wamesema fedha ambazo zimekuwa zikitumika kupigia debe ripoti ya BBI , zingesaidia kulipa wahudumu hao ambao wako katika mgomo.

Eddy Bahola katibu wa matabibu kaunti ya Lamu amesema tayari saini za BBI ,zimekusanywa na mamillioni ya fedha kutumika ,huku wao wakisalia bila kutiliwa maanani matakwa yao.

Ni siku zaidi ya 40 leo wahudumu wa afya kaunti ya Lamu ,wako katika mgomo wakilalamikia marupurupu ya kazi ngumu ,sawia na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na COVID 19.

Hali hiyo imesambaratisha huduma zote za afya, katika hospotali zote za umma Lamu, huku wagonjwa wakilazimika kusafiri hospitali zilizoko nje ya kaunti za kibinafsi kwa kusaka matibabu.