WAHUDUMU WA TUKTUK WALALAMA KUHUSU BARABARA MBOVU,VOI -TAITA TAVETA.


Wahudumu wa Tuk Tuk mjini Voi kaunti ya Taita Taveta ,wamelalamika vikali kuhusu ubovu wa barabara kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hivi majuzi.

Wahudumu hao wanasema kwa kipindi cha siku mbili sasa, baadhi ya maeneo yamekuwa hayapitiki ,hivyo kutoa wito kwa serikali ya kaunti kuingilia kati swala hilo.

Aidha wamelalama kuhusu utozwaji wa ushuru ,huku wakisema mwaka umekamilika.