Wahudumu wa mabasi Lamu hawataki kuandamana na polisi barabarani


Wahudumu wa mabasi ya abiria katika barabara kuu ya Lamu Witu na Garsen kaunti ya Lamu wametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuiondoa Escort katika barabara hiyo.

Kulingana na wahudumu hao Wamesema wanachukua muda mwingi barabarani kusubiri Escort, magari ya maafisa wa polisi kuwasindikiza kwa minajili ya usalama wa abiria na Mizigo yao.