WAHUDUMU WA AFYA WAPEWA SIKU SABA KURUDI KAZINI- TAITA TAVETA.


 

Wahudumu wa Afya wanaoshiriki mgomo katika kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kutekeleza agizo la Mahakama ,la kuwataka kutuma maombi yao kwa tume ya kuajiri wafanyikazi wa kaunti chini ya siku saba.

Kulingana na Waziri wa Afya wa Kaunti hiyo John Mwakima, Mahakama imeamuru Wahudumu hao kupeleka barua zao za maombi kwa tume ya kuajiri wafanyikazi wa kaunti ,kabla ya siku saba kukamilika.

Waziri huyo pia anasema kuwa katika uamuzi huo, serikali ya kaunti haijapewa masharti mapya na wanatarajia Wahudumu hao wa Afya kutekeleza agizo hilo la Mahakama .