WAHISANI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA CHAKULA


Wito umetolewa kwa wahisani kujitokeza ili kusaidia kamati ya kukabili virusi vya Corona kwa chakula kwani hadi sasa hakuna chakula cha nmsaada.
 
Kulingana na mwenyekiti wa kamati hiyo Ashok Anad anasema kwa sasa hawana chakula kwa akili ya familia ambazo zimeathirika kiuchumi kwani chakula kimeisha kwenye ghala.
 
Anand anasema maeneo ya miji ndio wameathirika zaidi kwa ukosefu huo wa chakula huku waklioko mashambani wakiwa na afadhali baada ya kupata mahindi walipolima.
 
Kwa sasa Ashok anasema wanalenga watu zaidi ya elfu moja mijini hasa waliokuwa wakifanya kazi katika sekta ya utaliii