WAGOMBEA WA UBUNGE WAAHIDI KUFANYA KAMPENI ZA AMANI, MSAMBWENI.


Wagombea wa kiti cha ubunge cha msambweni wameahidi kufanya kampeni za amani katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge hilo ulioratibiwa kufanyika tarehe 15 mwezi december mwaka huu

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kuziba pengo lililowachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Suleimani dori aliyefariki mwezi machi mwaka huu baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Wagombea hao tisa waliohudhuria kikao kilichoandaliwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu human rights agenda ,HURIA huko diani kaunti ya kwale, wamesema kuwa hawatachochea jamii kukagawinyika katika misingi ya kikabila na dini katika katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mdogo wa msambweni .

Wagombea hao ni pamoja na Feisal Dori , Sharlet Mariam, Mansoor kumaka, Charles Bilali , Omari boga , Shehe mahmoud ,Hamisi Mwakaonje ,Ali Hassan na Marere Mwachai .