Wafugaji wateta bei ya maziwa.


Changamoto imetolewa kwa serikali ya kaunti kupitia idara ya mifugo kusaidia wafugaji wa ng’ombe za maziwa kupata soko maalum kwani mara  kwa mara maziwa yao yamekuwa yakiharibika.

 
Kulingana na wafugaji hao kutoka nyanda za juu kaunti hiyo hasa maeneo ya Wundanyi wanasema wana uwezo wa kutoa lita elfu 60 kwa siku lakini tatizo lao kubwa ni kupata soko maalum.
 
Aidha wanasema bei ya sasa ya lita ya maziwa ya shilingi 35 hairidhishi  na kusema sharti serikali iwasaidie kupata wanunuzi wa bei nafuu.