Wafanyikazi kaunti ya Taita taveta kudai haki yao hata kwa Waganga.


Wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Taita Taveta wamesema watatumia kila mbinu hata kama nikuenda kwa waganga wa kienyeji ili kudai haki yao baada ya kuachishwa kazi.

Wafanyikazi hao wanasema licha ya kuhudumu katika vitengo mbalimbali vya serikali ya kaunti kwa zaidi ya miaka 15,kuachishwa kazi kulikua kwa madharau na kwamba hawakuhusishwa kikamilifu.

Wafanyikazi hao zaidi ya mia nne wengi wao wakiwa katika manispaa ya Voi wanasema tangu waachishwe kazi mwezi Januari hawaelezwa nini kilijiri huku pia wakisema watakabiliana na serikali ya kaunti mwaka 2022.

Haya yanajiri huku kukishuhudiwa upungufu wa vibarua katika hospitali sawa na wafanyikazi wa usafi katika miji ya kaunti hiyo.