Wafanyibiashara wafunga soko Lamu.


Wafanyabiashara zaidi ya 200 wa soko la Lamu Kisiwani Amu wametakiwa kufunga bihashara zao ikiwemo bidhaa kama vile Mboga,Matunda,Nyama sawa na nafaka na kurudi manyumbani ili kuepukana msongamano na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona….

Pendekezo la hapo awali kwa wafanyabihashara hao,walikuwa wamepewa muda wa siku tatu kuhamisha bidhaa zao katika uwanja wa Kibaki na kuendeleza kuuza bidhaa zao kabla ya kuamkia amri nyengine hii leo kutoka kwa idara ya usalama iliyowaamuru warudi manyumbani na bidhaa zao.

Ni takriban miezi sita sasa wafanyabiashara wa bidhaa za sokoni Lamu wamekuwa wakiuza bidhaa zao nje ya soko la Lamu katika bustani ya Mkunguni eneo la Lamu Fort ili kutoa nafasi ya ujenzi wa soko lao linaloendelea kujengwa upya na serikali ya kaunti.