Wabunge washabikia uamuzi wa kesi ya Mau


Hatua ya mahakama ya Nakuru kuzuia kwa muda wizara ya Mazingira na misitu kufurusha watu wanaokisiwa kuishi ndani ya msitu wa Mau kinyume na sheria imeshabikiwa na viongozi.

Mbunge wa kaunti ya Nakuru Liza Chelule amesema uamuzi huo utasaidia serikali na watu wanaolengwa kufurushwa kujadiliana na kujulishwa mahali mpaka wa msitu huo umefika.

Kauli ya Chelule aliyekuwa akizungumza katika eneo la Tendwet, Kuresoi Kusini imeungwa mkono na mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno.