Wabunge walalamikia barabara ya Dongo kundu.


Wahudumu wa bodaboda katika eneo la Tsunza kaunti ya Kwale wamelalamika kufungwa kwa barabara katika eneo hilo kufuatia ujenzi wa barabara ya Dongo Kundu katika eneo hilo.

Kulingana na Rama Ali Dziswa ambaye ni mhudumu wa boda boda katika eneo hilo ni kuwa barabara hiyo imefungwa bila wao kupewa taarifa yoyote jambo linaloathiri kazi zao.

Wakitishia kufunga eneo hilo ili kutoruhusu magari ya kampuni inayojenga barabara kuendelea na ujenzi huo.

Wakaazi hao wakilaumu viongozi wa eneo hilo kwa kutowasaidia licha ya madhila wanayopitia.