WABUNGE WA KITAIFA WATAKIWA KUISOMA NA KUICHAMBUA RIPOTI YA BBI ILI KUREKEBISHA VIPENGEE TATA-LAMU


Wabunge wa kitaifa kaunti ya Lamu wametakiwa kuisoma ripoti ya BBI na kuichambua kwa makini ,sawIa na kurekebisha vipengee tata vinavyomkandamiza mwanachi kabla ya kuipitisha katika bunge la Kitaifa.

Hii ni kufuatia hisia zilizoko kwamba huenda kaunti ya Lamu ,ikapoteza fedha nyingi ikiwa mswada wa BBI utapita ,kutokana na idadi chache ya watu walioko Lamu ambao ni watu walio chini ya laki mbili.

Aidha wakaazi wametoa wito kwa viongozi wao kuwaelimisha zaidi , kuhusu mswada wa BBI kwani hadi kufikia sasa wengi wao ,hawajui hasara na faida watakazopata kutokana na mswada huo.