WAALIMU NA WANAFUNZI WALALAMIKIA BARABARA MBOVU


Walimu na wanfunzi kutoka shule ya msingi ya kishamba kaunti ndogo ya mwatate wamelalamikia barabra mbovu yakuingia shuleni humo.

Kwa mahojiano na walimu kutoka maeneo hayo wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Ronald Mwaburi  amesema kuwa ubovu wa barabara hiyo ya kuingia shuleni humo hufanya wanafunzi wengi kuumia na kuchelewa hasa wakati wamvua inapo shuhudiwa kwani hakuna kivuko.

Wakati huohuo wamesema miundo msingi duni ya shule hiyo ya kishamba imechangia vile vile kuwa na matokeo duni kwa wanafunzi na kuitaka seriklai kupitia hazina ya kustawisha maeneo bunge kukarabatia majengio ya shule hiyo.