Vyuo vikuu vyafungwa kwa sababu ya Covid-19


Chuo kikuu cha Africa Nazarene kimefungwa kwa muda usiojulikana.

Naibu chansela wa chuo hicho Dk Stanley Bhebhe anasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza cha virusi vya Corona nchini kenya, mgonjwa akiarifiwa kutoka eneo la Rongai.

Kutokana na hilo, wanafunzi wameagizwa kuondoka shuleni hii leo ratiba ya mitihani ikiahirishwa.

Kwingineko chuo kikuu cha Riara kimeahirisha hafla ya mahafali iliyotarajiwa kufanyika juma lijalo.

Katika taarifa, naibu chansela wa chuo hicho Prof Robert gateru amesema kuwa uamuzi huo umeafikiwa kutokana na virusi vya Corona.

Hata hivyo shughuli za masomo zitaendeela kama kawaida.

Nacho Chuo kikuu cha Machakos kimekanusha madai kuwa kimefungwa.

Naibu chansela Prof Joyce Agalo amesema kuwa wameweka mikakati maalum iliyotangazwa na serikali hapo jana.