Vugu vugu na mchakatio wa kutafuta suluhu la ardhi.


Vuguvugu la jamii ya Mijikenda ukanda wa pwani maarufu kama Taireni, sasa limeanzisha mchakato wa kutafufa suluhu la ardhi ambazo zimenyakuliwa katika kaunti ya Lamu.

 

Katika taarifa yake mjini Malindi mwenyekiti wa Vuguvugu hilo Peter Ponda Kadzeha, amesema wakaazi wa eneo la Witu-Nyongoro, Wiitu-North na Nairobi Ranch kaunti hiyo wamekuwa wakihangaika kwa muda sasa.

 

Kulingana na Ponda muungano huo utatumia mbinu zote kikatiba ikiwemo kuelekea mahakamani ili kuhakikisha kwamba wakaazi wa sehemu hiyo wanapata ardhi yao.