VITA DHIDI YA UKEKETAJI KAUNTI YA TANA RIVER


Wadau katika vita dhidi ya ukeketaji wa wasichana kule Tanariver sambamba na viongozi eneo hilo sasa wanadai kuwa ukeketaji umepungua kwa asilimia kubwa.

Kulingana na wadau hao akiwemo mwakilishi wa akina mama kaunti ya Tanariver Rehema Hassan ukeketaji umepungua kutoka asilimia 100 ya hapo awali hadi 60 hivi sasa.

Wadai hao wanahoji kuwa hatua hiyo imetokana na kushirikishwa kwa washikadau mbali mbali katika vita hivyo sambamba na mbinu kochokocho ikiwemo michezo miongoni mwa vijana.

Kwa sasa washirikishi wa vita dhidi ya jinamizi hilo wanafichua kuwa tayari vijana katika eneo hilo wamekubali kuoa wasichana ambao hawajakeketwa ili kuchangia kupiga vita hivyo.