VISA VYA DHULMA VIRIPOTIWE KWA WAKATI


Wito umetolewa kwa wazazi wa kaunti ya Taita Taveta  hususan kina mama, kuripoti visa vya dhuluma za kimapenzi mapema iwekanavyo kwa minaajili ya  hatua zifaazo kuchukuliwa.

Kulingana na wenyekiti wa sauti ya wanawake eneo la mwangea mjini voi Macrina Mwamburi, amesema ni sharti visa hivyo kuripotiwa mapema, kwa lengo la kujali afya ya mwathiriwa.

Wakati uo huo ameongeza kuwa utoaji wa habari kuhusiana na visa hivyo kutasaidia kupunguza maovu hayo yanayoendelea kushuhudiwa katika kaunti hiyo.