Visa vya corona hatari kwa wakaazi wa Nakuru- Lee


Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui ameonya wakaazi dhidi ya kulegeza masharti ya kuzuia virusi vya corona.

Tangu serikali iondoe marufuku ya kutosafiri kutoka kaunti moja hadi nyingine, nakuru imeshuhudia ongezeko la hadi asilimia 86 ya virusi vya corona hii ikijumuisha visa 2,020.

Kinyanjui aliyekuwa akizungumza na runinga ya Citizen ameonya kuwa huenda masharti makali yakatolewa ili kuzuia visa zaidi.